IQNA

Kiongozi wa Hizbullah

Marekani inaenza chuki dhidi ya Iran ili kuzuizia silaha nchi za Kiarabu

20:38 - October 13, 2018
Habari ID: 3471706
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani anatumia sera ya kueneza propaganda chafu dhidi ya Iran kwa shabaha ya kutaka kuuza silaha za mabilioni ya dola kwa nchi za Kiarabu.

Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa serikali zilizotangulia za Marekani zilikuwa zikipora utajiri wa nchi mbalimbali kwa njia za kidiplomasia na kwa heshima lakini sasa Donald Trump anaiba na kupora utajiri wa nchi hizo waziwazi na kwa madharau na jeuri.

Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah amezitaka nchi za Waislamu zipate ibra na funzo kutokana na matamshi ya dharau yaliyotolewa na Donald Trump akisema kuwa kama si Marekani basi watawala wa Saudi Arabia hawawezi kubakia madakani walau kwa kipindi cha wiki mbili.

Sayyid Nasrullah ameshiria jibu la nchi za Kiarabu kwa matamshi hayo ya Trump dhidi ya Saudi Arabia wakiwemo viongozi wa serikali ya Riyadh wenyewe na kusema: Watawala wa nchi za Kiarabu walipokea madharau hayo ya Trump kwa tabasamu, udhalili na kunyamaza kimya.

Vilevile ameashiria matamshi yaliyotolewa na Rais wa Marekani kwamba Iran ilikuwa na mpango wa kuzidhibiti nchi za Mashariki ya Kati katika kipindi cha dakika 12 tu na kusema: Matamshi hayo yanatolewa kwa ajili ya kuwalazimisha viongozi wa nchi za Kiarabu watowe pesa zaidi kwa Marekani kwa ajili ya kulinda tawala zao.

Amesema Iran kamwe haina mzaha na yeyote katika kulinda uslama wake na kwamba matamshi hayo ya Trump yanaonesha adhama na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu. 

Amesema kwamba Trump anaitambua Jamhuri ya Kiislamu kuwa ni nchi kubwa na yenye nguvu na kuziona nchi za Kiarabu zinazonunua silaha za mabilioni ya dola kutoka Marekani kuwa ni dhaifu kiasi kwamba watawala wao hawawezi kubakia madarakani walau kwa masaa 12 bila ya msaada na himaya yake. 

3466958

captcha