IQNA

Iran kuandaa kongamano la ‘Mustakabali wa Ulimwengu wa Kiislamu’

21:48 - October 09, 2018
Habari ID: 3471705
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza mpango wa kuandaa kongamano la ‘Mustakabali wa Ulimwengi wa Kiislamu Kufikia Mwaka 2035.’

Kongamabo limepangwa kufanyika katika Kitivo cha Sheria na Sayansi ya Kisiasa katika Chuo Kikuu cha Tehran kuanzia Machi 28-29.

Mada muhimu zitakazo jadiliwa ni pamoja ustawi wa kijamii katika ulimwengu Kiislamu, mustakabali wa uchumi wa uchumi wa ulimwengu wa Kiislamu, mustakabali wa siasa na usalama wa ulimwengu wa Kiislamu, mustakabali wa sayansi na teknolojia katika ulimwengu wa Kiislamu na mustakabali wa ustaarabu, utamaduni na thamani za ulimwengu wa Kiislamu.

Wanaokusudia kushiriki katika kongamano hilo wanapaswa kutuma muhtasari wa makala zao Oktoba 22 na makala kamili kabla ya Disemba 6.

Kongamano hilo limeandaliwa na Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO), Chuo Kikuu cha Allameh Tabatabei, Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na Chuo Kikuu cha Imam Sadeq AS.

3754098

captcha