IQNA

Wanazi mamboleo wauhujumu msikiti Ujerumani

17:37 - October 02, 2018
Habari ID: 3471699
TEHRAN (IQNA)- Msikiti mmoja umehujumiwa huko Ujerumani katika mji wa Gladbeck katika jinai ambayo inasadikiwa imetekelezwa na wanazi mamboleo wanaowachukia Waislamu.

Kwa mujibu wa taarifa genge la wabaguzi waliuhujumu msikiti huo ulio kaskazini mashariki mwa Ujerumani na ambao unasimamiwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Masuala ya Kidini Uturuki (DITIB). Nadir Kahraman, mkuu wa DITIB tawi la Gladbeck amelaani hukuma hiyo na kutoa wito kwa maafisa wa usalama kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahusika.

Amebainisha masikitiko yake kuwa kwa muda mrefu sasa misikiti imekuwa ikihujumiwa na wabaguzi mara kwa mara lakini hakuna hatua ambazo huchukuliwa. DITIB ni taasisi ambayo imeanzishwa na Wajerumani wenye asili ya Uturuki na inasimamia misikiti 900 kote Ujerumani.

Ujerumani ni nchi yenye watu milioni 81 na ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu Ulaya maghairbi baaada ya Ufaransa. Waislamu Ujerumani wanakadiriwa kuwa milioni 4.7 ambapo milioni 3 miongoni mwao wana asili ya Uturuki.

3466880

captcha