IQNA

Qarii wa Iran ashinda Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Croatia

20:16 - September 30, 2018
Habari ID: 3471697
TEHRAN (IQNA)- Qarii (msomaji wa Qur'ani) ameibuka mshindi katika Mashindano ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Croatia yaliyomalizika Jumamosi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Qarii Kazem Azar-Pira wa Iran alichukua nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na mwakilishi wa Uturuki.
Mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu yalikuwa na washiriki 75 kutoka nchi 42.
Mwaka 2016 pia, mwakilishi wa Iran katika kategoria ya qiraa alishika nafasi ya pili.

 

Qarii wa Iran ashinda Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Croatia

3751280

captcha