IQNA

Afrika Kusini yasisitiza kuhusu sera zake dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel

9:32 - September 29, 2018
Habari ID: 3471695
TEHRAN (IQNA)- Afrika Kusini imesisitiza kuwa sera zake dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel zinabaki pale pale.

Kauli hiyo imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini baada ya kubainika kuwa balozi wa nchi hiyo amerejea mjini Tel Aviv. Katika taarifa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imesema Balozi Sisa Ngombane alifika Israel kwa ajili ya kazi za kibinafsi.
Mapema mwaka huu serikali ya Afrika Kusini ilisema itapunguza kiwango cha uhisiano wake na Israel kutoka kiwango cha ubalozi hadi kiwango cha ofisi ya uratibu kufuatia uamuzi uliochukuliwa na chama tawala ANC. Baada ya uamuzi huo Afrika Kusini ilimuita nyumbani Balozi Ngombano kutoka Tel Aviv mwezi Mei baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwaua shahidi Wapalestina 40 katika maandamano ya amani huko Gaza.
Mapema wiki hii mbunge wa ngazi za juu wa ANC, Nkosi Mandla, mjukuu wa Shujaa Nelson Mandela, alikosia serikali kwa kumruhusu Ngombane kwenda Israel kwa siri.
AIdha chama cha EFF kimekituhumu chama cha ANC kwa kusitisha uungaji mkono wa harakati za ukombozi wa Palestina.
Mwezi Disemba mwaka jana Chama tawala cha Kongresi ya Taifa cha Afrika Kusini (ANC) kilitangaza katika mkutano wake wa kitaifa kuhusu kushusha hadhi ya uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Isarel. Mkutano wa taifa wa chama tawala ANC, ambao unatambulika kama kikao cha ngazi ya juu cha kutoa maamuzi ya chama kwa sauti moja uliamua kuchukuliwa haraka na bila ya masharti yoyote hatua ya kushusha hadhi ya ubalozi wa Afrika Kusini huko Israel na kuwa ofisi tu ya uratibu.

/3750754

captcha