IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kaaba Tukufu, Masjid Al-Haram, na Masjid An- Nabawi ni ya Waislamu wote

21:43 - July 16, 2018
Habari ID: 3471596
TEHRAN (IQNA) –Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesisitiza kuwa misikiti miwili mitukufu zaidi katika Uislamu ni ya Waislamu wote duniani.

Ayatullah Khamenei amesema hayo leo asubuhi mjini Tehran alipokutana na maafisa wa kusimamia ibada ya Hija wa nchini Iran ambapo aliongeza kuwa: "Kaaba Tukufu, Masjid Al-Haram, na Masjid An- Nabawi ni ya Waislamu wote na wala si milki ya watu wanaotawala maeneo hayo."

Ayatullah Khamenei amesema hakuna mtu mwenye haki ya kuzuia kufikiwa ufahamu halisi wa Hija na iwapo kuna utawala au serikali itakayofanya hivyo basi kitendo hicho kitakuwa ni  'sad an Sabilillah' kwa maana ya kuwazuia waja katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kiongozi Muadhamu alikuwa akiashiria aya ya 25 ya Sura Hajj isemayo: "Hakika wale walio kufuru na wakazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu na Msikiti Mtakatifu, ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni. Na kila atakayefanya upotofu humo kwa dhulma, basi tutamwonjesha adhabu chungu."

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Hija halisi inapaswa kujumuisha  Baraaat min-al-Mushrikeen yaani a kujibari na kujitenga na washirikina sambamba na kuanzaa mazingira ya umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu duniani.

Akiashiria maafa ya Mina ya waka 2015 ambapo maelfu ya Mahujaji walipoteza maisha, Ayatullah Khamenei amesisitiza ulazima wa kufuatilia kadhia hiyo ili kuhakikisha fmailia za waathrika zinapata haki.

Kwingineko katika hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema siasa za kishetani za Marekani kuhusiana na Palestina kamwe hazitafanikiwa.

Kiongozi Muadhamu ameashiria jinsi maadui walivyojizatiti kwa ajili ya kukabiliana na Waislamu hususan kadhia ya Palestina na masuala yanayohusiana na Yemen na kubainisha kwamba, hivi sasa Marekani imezipa siasa zake za kishetani kuhusiana na Palestina jina la 'Muamala wa Karne', lakini wanapaswa kutambua kwamba, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, muamala huo wa karne katu hautafanikiwa kufikia malengo yake na viongozi wa Marekani hawatafanikiwa kuushuhudia kwa macho yao mpango huo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kadhia ya Palestina haitasahaulika na Quds utabakia kuwa mji mkuu wa taifa la Palestina.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, taifa la Palestina litasimama imara mbele ya njama za maadui na mataifa ya Kiislamu nayo yataliunga mkono taifa madhulu la Palestina.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amebainisha wazi kwamba, baadhi ya madola ya Kiislamu ambayo tab'ani hayana imani na Uislamu, yamejitolea kwa ajili ya Wamarekani kutokana na ujinga, ujahili na tamaa za dunia yaliyonayo; hata hivyo kwa tawfiki ya Mwenyezi Mungu, Umma wa Kiislamu na taifa la Palestina watawashinda maadui na wataishuhudia ile siku ambayo mizizi ya utawala bandia wa Israel itakapong'olewa katika ardhi za Palestina.

3466288

captcha