IQNA

Iran Kutuma Msafara wa Qur'ani katika Ibada ya Hija

14:54 - July 12, 2018
Habari ID: 3471591
TEHRAN (IQNA)- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa itatuma msafara wa Qur'ani Tukufu, katika Ibada ya Hija mwaka huu nchini Saudi Arabia.

Msafara huo ambao ni maarufu kama 'Msafara wa Nur', utashiriki katika vikao mbali mbali vya Qur'ani Tukufu katika miji ya Makka na Madina.

Akizungumza katika kikao cha washiriki wa msafara huo Jumatano, Mohammad Taqi Mirzajani, mkuu wa Kamati ya Kutuma Wasomaji Qur'ani Nchi ya nchi amesema Msafara wa Nur mwaka huu utakuwa na Maqarii (wasomaji) na Mahuffadh (waliohifadhi)  19 wa Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, msafara huo huo utaongozwa na Ustadh Ahmad Abul Qasemi.

Kila mwaka Iran hutuma wasomaji wa Qur'ani katika Ibada ya Hija Saudia Arabia na huwa wanashiriki katika vikao na mahafali za Qur'ani Tukufu.

Wairani zaidi ya 85,000 wanatazamiwa kujinga na mamilioni ya Waislamu katika kutekeelza Ibada ya Hija mwaka huu.

 

3466264

captcha