IQNA

Msichana wa Kwanza Kufika Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Rwanda

13:03 - July 09, 2018
Habari ID: 3471588
TEHRAN (IQNA)-Binti Aisha Nikuze amekuwa msichana wa kwanza kufika katika fainali ya Mashindano ya 7 Kimataifa ya Qur'ani ya Rwanda yaliyofanyika mwezi uliopita.

Aisha aliweka rekodi hiyo katika mashindano hayo ambayo yaliwaleta pamoja wanafunzi 43 kutoka nchi 17 za Afrika. Aghalabu ya washiriki waliondolewa katika mchujo ni ni 19 tu walioingia katika duru ya pili ambapo Nikuze aliibuka wa tatu ni akawa mshiriki pekee wa kikei kuwahi kufika katika fainali ya mashindano hayo tokea yaanzishwe miaka saba iliyopita.
Nikuze ni mtoto wa kwanza na mtoto pekee wa kike wa Saada Kananura na Fatuma Nikuze.
Alimaliza masomo yake ya shule ya upili mwaka 2015 katika shule ya Ecole Secondaire Scientifique Islamique huko Nyamirambo lakini hakuweza kuendelea na masomo ya juu kutokana na uhaba wa fedha.
Nikuze anasema alihimizwa na wazazi wake kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka mine na alipata motisha wa kusoma na hatimaya akafanikwa kufikia lengo lake.
Nikuaze ameshiriki katika pia katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani mwaka jana mjini Dubai ambapo pia alifanya vizuri. Anasema kuhifadhi Qur'ani kumemsaidia katika kuishia maisha bora na wengine kwa amani, mapenzi, umoja na maelewano.
Baba yake Nikuaze, Kananura, anasema alimhimiza sana binti yake kuhifadhi Qur'ani Tukufu na hivyo anafuraha kuwa ameweza kufanikiwa.

3466237/

captcha