IQNA

Msikiti wa Kwanza Kufunguliwa Hebrides, Scotland, Kanisa Lapinga

11:43 - April 10, 2018
Habari ID: 3471460
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa kwanza kujengwa katika eneo la Outer Hebrides huko Scotland nchini Uingereza utafunguliwa katika kipindi cha miezi michahce ijayo hata baada ya Kanisa la Presbyterian kupinga vikali ujenzi huo.

Waislamu walichanga  £56,000 kujenga msikiti huo ikiwa ni zaidi ya lengo lao la kuchangisha £50,000 na tayari kibali cha uzinduzi kimashatolewa.

Uzinduzi wa msikiti huo umekumbwa na upinzani mkubwa wa Kanisa la Presbyterian Free la Scotland ambalo limetoa wito kwa wafuasi wake kushiriki katika maombi maalumu ya kuhakikisha msikiti huo hautajengwa.

Mpango wa uzinduzi wa msikiti huo unaongozwa na Aihtsham Rashid ambaye ni mjenzi kutoka eneo la Leeds Uingereza. Anasema kuna Waislamu wengi wenye asili ya Syria katika eneo hilo ambao wametaka msikiti uanzishwe. Kwa mujibu wa sense ya mwaka 2011 kulikwa na Waislamu 61 na Wakristo 20,452 katika eneo hilo la Outer Hebride,s ambalo pia linajulikkana kama Western Isles. Idadi ya  Waislamu imeongezeka kwa kasi tokea wakati huo na sasa kuna haja ya kujengwa msikiti katika eneo hilo. Waislamu wamenunua nyumba ya kale ambayo itakarabatiwa na kugeuzwa kuwa msikiti. Kasisi David Blunt wa kanisa la eneo hilo amebaini wasiwasi wake kuwa Uislamu utaenea zaidi katika eneo hilo iwapo msikiti utajengwa.

3704270

captcha