IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa

Marekani na waitifaki wake ni wachochezi wakuu wa fujo, ghasia Iran

22:20 - January 05, 2018
Habari ID: 3471343
TEHRAN- (IQNA) Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema, fujo ambazo zimeshuhudiwa siku za hivi karibuni mjini Tehran zinaashiria kuwepo uchochezi wa Marekani na vibaraka wake.

Katika siku kadhaa zilizopita, baadhi ya watu kwenye miji kadhaa humu nchini walifanya mikusanyiko na maandamano kulalamikia masuala mbalimbali ikiwemo kutojulikana hatima ya watu waliopata hasara na kupoteza fedha zao katika taasisi za fedha, ughali wa baadhi ya bidhaa na udhaifu wa serikali katika usimamizi wa mambo.

Hata hivyo baadhi ya maandamano hayo yalitumiwa vibaya na watu wenye nia mbaya na wahuni wanaoungwa mkono na baadhi ya nchi za Magharibi, za Kiarabu na utawala wa Kizayuni wa Israel kuzusha fujo na machafuko.

Kufuatia fitina hiyo, tokea siku ya Jumatano, wananchi wa Iran katik amiji mbalimbali humu nchini wamekuwa wakishiriki katika maandamano makubwa ya kulaani njama hizo za maadui na wahuni waliotumia fursa hiyo kuharibu mali za umma.

Katika hotuba zake za Sala ya Ijumaa ya leo, Ayatullah Sayyed Ahmad Khatami amesema baada ya Marekani na waitifaki wake kushindwa mara kadhaa katika eneo hili ikiwemo katika vita vya Syria na Iraq, sasa wamekuwa wakitafuta fursa mpya ya kutoa pigo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo iko katika mstari wa mbele kwenye kambi ya muqawama.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameongeza kuwa, Marekani na waitifaki wake walikuwa wanadhani kuwa, kwa kuunga mkono wahuni na wazusha fujo, wangeliweza kutoa pigo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lakini taifa la Iran lenye busara, muono wa mbali na welewa mkubwa, sawa na miaka ya huko nyuma, mara hii pia limejitokezwa kwa wingi na kuleta hamasa ya aina yake ambayo imesambaratisha njama hizo za Marekani na waitifaki wake.

Maandamano ya wananchi

Wakati huo huo, wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya Sala ya Ijumaa wameshiriki kwenye maandamano makubwa katika maeneo mbali mbali nchini, ukiwemo mji mkuu Tehran, kulaani fujo na ghasia zilizozushwa hivi karibuni huku wakitaka wahusika wa fitina hizo wachukuliwe hatua kali kisheria.Marekani na waitifaki wake ni wachochezi wakuu wa fujo, ghasia Iran

Aidha waandamanaji wamesisitiza kuhusu ulazima wa kukabiliana na fitina zilizozushwa na Marekani na waitifaki wake. Washiriki wa maandamano hayo wametoa nara za "Mauti kwa Marekani" na "Mauti kwa Israel" huku wakiteketeza bedera za tawala hizo mbili. Waandamanaji hao pia wametoa nara za "Mauti kwa Aal Saud" na kuulani utawala wa Saudia kwa kushirikiana na Wamarekani na Wazayuini kuchochea fitina na ghasia nchini Iran.

captcha