IQNA

Waziri wa Elimu Austria apinga Hijabu, Waislamu wasema huo ni mstari mwekundu

15:06 - December 30, 2017
Habari ID: 3471332
TEHRAN (IQNA)-Waislamu nchini Austria wamekosoa matamshi dhid iya vazi la Hijabu ambayo yametamkwa na waziri mpya wa elimu Heinz Fassmann.

Katika mahojiano siku ya Ijumaa na gazeti la Kurier, Fassmann alinukuliwa akisema: “Walimu hawapaswi kuvaa Hijabu.”

Alipoulizwa kuhusu marufuku ya Hijabu, Fassmann alisema: “Naam, naunga mkono dola la kisekula (lisilozingatiamisingiyakidini) na naamini walimu hawapaswi kuvaa Hijabu isipokuwa wale waliokatikashulezakidininabinafsi.”

Serikali ya mseto Austria iliyoundwa mapema mwezi huu na inayojumuisha chama cha Watuwa Austria (OVP) na chama chenye misimamo mikali ya kibaguzi cha mrengo wa kulia, Freedom Party (FP0) ni serikali yenye misimamo dhidi ya Uislamu na dhidi ya wahamiaji.

Kufuatia matamshi hayo yaFassmann, mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu la Austria (IGGO) Ibrahim Olgum amesema, “Hijabu ni mstari mwekundu.”

“Tunafikiri kuwa azma ya kupiga marufuku Hijabu inatokana na misimamo iliyo dhidi ya Uislamu,” ameongeza Olgun.

Kwa upande wake KatibuMkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Vienna (IFW) Harun Eciyas amesema: “Kudai kuwa walimu wanaovaa Hijabu wanakiuka msingi wa kutopendelea upande wowote kuna maana ya kuvunjia heshima elimu na kazi yao. Bila shaka tutapinga msima mohuo.”

Ameendelea kusema kuwa: “Hijabu ni sehemu ya Uislamu na kwa msingi huo ukipiga marufuku Hijabu katika idara za serikali ni sawa na kuwafukuza Waislamu kutoka sehemu za umma na huo bila shaka ni ubaguzi.”

Januari mwaka huu Sebastian Kruz ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Utangamano wa Austria alitoawito wa kupigwa marufuku vazi la stara la Hijabu linalovaliwa na wanawake Waislamu katika maeneo ya umma nchini humo.

Alisema kuwa anaandaa muswada ambao ukipasishwa na kuwa sheria, wanawake wa Kiislamu nchini humo na hususan wafanyakazi wa umma kama vile walimu hawataruhusiwa kufunika vichwavyaowakiwakazini.

Hivi sasa Kruz niKansela wa Austria, cheo ambacho ni sawa na cha rais, na hivyo kuna wasiwasi mkubwa kuwa atatekeleza sera hizo zilizo dhidi yaWaislamu.

3464792

captcha