IQNA

Nalaka za Qur'ani zatupwa mtaro wa maji taka mjini Taif, Saudi Arabia

11:41 - October 21, 2017
Habari ID: 3471224
TEHRAN (IQNA)-Idadi kubwa ya nakala za Qur'ani zimepatikana hivi karibuni zikiwa zimetupwa katika mtaro wa maji taka katika mtaa mmoja katika mji wa Taif, Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa tovuti ya aljarida.com ya Tunisia, mvulana mwenye umri wa miaka 13 alipata nakala hizo za Qur'ani na kumjulisha baba yake ambaye aliripoti katika kituo cha polisi.

Kanali kadhaa za televisheni zimeonyesha taswira ya video ya nakala za Qur'ani zikiwa zimetapakaa barabarani baada ya kuondolewa katika mtaro wa maji taka mjini Taif jambo ambalo limeibua hasira miongoni mwa Waislamu kote duniani.

Matukio ya kuvunjia heshima nakala za Qur'ani yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara nchini Saudi Arabia. Mwaka 2013 nakala zingine za Qur'ani zilipatikana katika mabomba ya maji taka mjini Taif. Aidha mwaka jana katika gereza ya Al-Ha'ir kuliibuka ghasia miongoni mwa wafungwa baada ya afisa wa jela kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu.

Mwaka 2016 ubalozi wa Saudia Arabia nchini Morocco ulikosolewa vikali na Waislamu baada ya kuenea picha za kuvunjiwa heshima nakala za Qur'ani Tukufu katika ubalozi huo.

Waislamu katika mitandao ya kijamii wamebainisha ghadhabu na hasira zao dhidi ya Utawala wa Saudia kufuatia kitendo cha wanadiplomasia wake kuonyesha kutoheshimu hata kidogo nakala za Qur'ani Tukufu.

Matukio ya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu Saudi Arabia yanaajiri katika hali ambayo nchi hiyo ni mwenezaji mkuu wa itikadi ya Uwahhabi na ukururishaji Waislamu wasiokubali itikadi hiyo duniani.

3654900

captcha