IQNA

Magaidi wa Kikrsito waua Waislamu 25 katika Msikiti CAR

12:53 - October 14, 2017
Habari ID: 3471216
TEHRAN (IQNA)-Magaidi wa Kikristo wa kundi la anti-Balaka wameua Waislamu 25 ndani ya msikiti katika mji wa Kembe kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Magaidi hao waliuzingira na kuushambulia msikiti huo mapema Jumatano asubuhi, amesema Abdourahman Bronou, mkuu wa baraza la wazee katika mji wa Kembe.

Akizungumza Ijumaa, Bornou ameongeza kuwa, katika hujuma hiyo ya kigaidi Imamu wa msikiti na naibu wake walikuwa miongoni mwa waliouawa. Wakuu wa mji huo wametangaza siku tatu za maombolezo.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) yaliibuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo,François Bozizé. Baada ya rais Mwislamu, Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi na magaidi wa Kikristo wenye kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu waliuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi.

Djotidia alilazimishwa na nchi za kieneo kujiuzulu Janarui mwaka 2014 na hapo mauaji ya Waislamu yakashika kasi zaidi. Kabla ya kuanza mgogoro, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui, ulikuwa na wakaazi 130,000 Waislamu lakini sasa taarifa zinasema idadi hiyo ni chini ya 1,000.

Aidha watu zaidi ya 400,000, wengi wakiwa ni Waislamu wamelazimika kukimbia makazi yao huki wengine milioni 2.7, au nusu ya watu wote CAR wanahitaji msaada. Mauaji ya Waislamu CAR yanajiri pamoja na kuwepo vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini humo.

3652446

captcha